Tuesday, December 27, 2011
IZO B na Barnaba wakisanua Villa Park pia...!!
Wakati Barnaba akitoka stage kuwarusha mashabiki na track kama Daima Milele,Tulizana na ngoma nyingine kali huku masista duu kibao wakioneka kupagawa na ngoma zake pamoja na presentation bab kubwa,
Izo B nae alikisanua na ngoma kama Miss Business,Business na Naongea na Ridhiwan ngoma ambayo ilifanya watu kumtunza kwa pesa,huku akiendeleza harakati za kuitambulisha track mpya BARUA,ambayo ni muendelezo wa RIDHIWANI...!!!
Linah on STAGE na Mwana FA wa MWANZA
Linah a.k.a ndege mnana kutoka THT,ndani ya Villa Park Resort alizua SHANGWE ghafla kwa mashabiki waliohudhuria show pale alipotaka kuperform nyimbo alioimba na Mwana FA "YALAITI"
Huku akitumia mfumo wa PLAY BACK aliomba mtu mmoja apande on stage na aimbe sehemu ya FA,ndipo mchizi alipopanda na kuanza kuchezesha taya huku akitupia swaga za FA,Crowd iliripuka baada ya mchizi kumbambia Linah..!!
Sauti ya Linah haikumpa Support hata kushindwa kuimba live kama ilivyo ada yake..!aliomba radhi kwa sauti kumgomea na mashabiki walionekana kumuelewa.
Monday, December 26, 2011
Bata za x-mas
Baraka wa Mwanza Rainbow,Ben Tv presenter at Star Tv na mchumba wake Magie'pia walikuwepo katika uzinduzi wa album ya HILLWAY BAND "BOMU LIMELIPUKA"
Barnaba na Ezden the Rocker
Rock city super star Ezden the Rocker,rapper and Radio presenter at KISS FM along side with Barnaba wakishow luv mbele ya Camera ya Mwanza Rainbow blogspot.Ni katika uzinduz wa HILLWAY BAND ndani ya ukumbi wa GOLD CREST.
Uzinduzi wa HILLWAY BAND waingia DOSARI.
Uzinduzi wa Band ya HILLWAY a.k.a Wazee wa juu kwa juu,uliofanyika jana usiku wa x-mas katika ukumbi wa GOLD CREST ,ulingia dosari baada ya wasanii walioalikwa"ROMA MKATOLIKI na BELLE 9" kutopanda stage on time ,hivyo kusababisha waandaaji kutowaruhusu wasaani hao kuperform ,baadhi ya watu walioingia katika uzinduzi huo walionekana kukasirishwa na kitendo hicho na kuomba kurudishiwa pesa zao kwani si wote walikuja kwa ajiri ya kuangalia uzinduzi bali Bongo fleva arists,Roma na Belle 9.
Tofauti na dosari hiyo HILLWAY BAND,walifanikiwa kuwakonga nyoyo mashabiki wa mziki wa dansi Mwanza huku wakiuza VCD ya ALBUM yao ya BOMU LIMELIPUKA kwa tshs. laki moja na ishirini kwa mdau wa mziki huo..!
Sunday, December 25, 2011
IZO B v/s Mwanza Rainbow Dancers
Happy Birthday IZO B,
Wakati akitimiza miaka kadhaa leo,Izo biashara kasema na Ridhiwan ndani ya jiji la Mwanza huku akitambulisha ngoma mpya"BARUA" ambayo ni muendelezo wa Naongea na RIDHIWANI...!bonge la ngoma bonge ya show...!bravo
Barnaba v/s Mwanza Rainbow Dancers
Uchache wa watu uliojitokeza katika show hii,leo siku ya x-mas haikuwa kigezo cha kumfanya Barnaba kufanya show nzuri huku akipewa support ya kutosha kutoka kwa dancers wa Mwanza Rainbow,haina ubishi kuwa yeye ni muimbaji na performer....!!Zaid ya saa moja akiwa on stage akikisanua nonstop huku baadhi ya mashabiki wakimtuza..!
Barnaba na Baraka waki-holla kabla ya show.!!
Msanii wa mziki wa kizazi kipya,Barnaba boy a.k.a kipenzi cha mabinti,ambaye ni zao toka nyumba ya vipaji Tanzania THT akiholaa na Baraka,Creative Director wa Mwanza Rainbow Academy of Art kabla ya show,ndani ya uwanja wa Ccm Kirumba Mwanza...!!
Sunday, December 18, 2011
NEW STARS ARISINNG
Check out this pic..'naamiini utaafiki this two gals "Juliet na Alinda" ni NYOTA mpya katika Bongo Movie industry.Moja ya scene katika movie ya "SAFARI YA MTOTO KADIBO"
Mwanza City
So Fresh so Clean,beautiful city'full of Rocks.....!you can call it ROCK CITY'the city of SATO
Karibu Mwanza and Enjoy
Saturday, December 17, 2011
MAHAFARI YA 46 CBE
Maandalizi ya Mahafari ya Chuo cha biashara Campas ya Mwanza,mvua za hapa na pale zinaonekana kukwamisha shughuli kuanza katika wakati muafaka.
Friday, December 16, 2011
SAFARI YA MTOTO KADIBO, in the making
- Nasimento,Kadibo na Bomba wakiwa mtaani wakiaomba katika daladala,Moja ya ratiba zao za kila siku katika harakati za kujipatia mkate wa kila siku.
- Kisteza na mwezake wakifuta magari mtaani pia katika mishe za kusaka mahela.
- Director Souzy'mwenye boom'na Barry "mweny Camera-creative director wa Mwaza Rainbow.
Thursday, December 15, 2011
Full Bata this holiday....!
Denimah Enterprises na Midland Hotel watakinukisha this holiday kwa kuwaleta artist wakali katika kuitambulisha HILLWAY BAND,Artist watakaokisanua pande za Mwanza,Geita,Musoma na Bukoba ni Pamoja na Tundaman,Richard,Roma Mkatoliki ,Kabago na Dancers kutoka Mwanza Rainbow Acaademy of Art.
Tuesday, December 13, 2011
Fashion in Mwanza
Fashion industry inazidi kukua kwa kasi katika jiji la Mwanza,Models kutoka MWANZA RAINBOW ACADEMY OF ART,during photo shooting.J-model,Jessy and Ritchie.I hope ni channel nyingine nzuri kwa makampuni na wafanya biashara jijini Mwanza kuwatumia katika kutangaza bidhaa zao...!
Monday, December 12, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)