Friday, January 25, 2013

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA KAMANDA AELEZA WALIVYOJIFICHA MAKABURINI BAADA YA KUFANYA MAUAJI

Abdurahman Ismail aka Dulla (28) ambaye ni mkazi wa Mkudi Ghana jijini Mwanza ambaye ni mdogo wa watuhumiwa Muganyizi Michael Peter aliyedaiwa kumfyatulia risasi marehemu Barlow alieleza jinsi walivyo tekeleza unyama wao na kwenda kuficha radio call na funguo za gari kwa kutupa katika tankila maji taka katika eneo la Nyashana kwenye nyumba ambayo haina mahusiano yoyote na hao watuhumiwa bali kwa lengo la kuhakikisha vitu hivyo havipatikani kabisa.

Watuhumiwa wawili waliofungwa pingu wakiwa wameshikiliwa na makachero wa jeshi la polisi waliovalia kiraia wakiwaonyesha kwenye shimo la maji taka eneo ambalo walitupa Radio call pamoja na funguo za gari la aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza marehemu Liberatus Barlow.

Watu hao walitumbukiza radio call hiyo na funguo za gari kupitia bomba linaloonekana kulia la kupitishia hewa ya maji taka na hapa ni harakati za kutindua mlango wa shimo la maji taka lililotajwa kuwa na radio call na ufunguo wa gari la vilivyokuwa vikitumiwa na marehemu Barlow siku ya tukio la mauaji yake eneo la minazi mitatu Kitangili wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza (RCO) Joseph Konyo akijiandaa kuchungulia ndani ya shimo la maji taka lililotajwa kuwa na radio call na ufunguo wa gari la vilivyokuwa vikitumiwa na marehemu Barlow siku ya tukio la mauaji yake eneo la minazi mitatu Kitangili wilayani Ilemela jijini Mwanza.

                                               Picha ya ndani ya shimo hilo..

                                          Funguo za gari zikifanyiwa usafi..

Hivi ni baadhi ya vitu vilivyokamatwa nyumbani kwa watuhumiwa hao vikiwemo vyeti vya kughushi, pasipoti na picha za utambulisho wa kughushi wa kipolisi, simu zaidi ya nne zenye laini zake na laini nyingine za ziada kwa mitandao tofauti, sare za moja kati ya makampuni ya ulinzi Mwanza, kofia zenye nembo ya jeshi la Polisi na kadhalika...

 

No comments:

Post a Comment