Tuesday, January 15, 2013

MEYA WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA AVUNJA REKODI KWA KUVUNJA MIPAKA YA SIASA



Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangiri Henry Matata akihutubia wananchi katika uwanja wa wazi wa Kitangiri jijini Mwanza uliokuwa na lengo la kuwasilisha shughuli za utendaji wa kata yake sambamba na kufafanua mikakati iliyopo juu ya masuala mbalimbali ya maendeleo kwenye kata hiyo.




Meya wa Ilemela henry Matata ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangiri jijini Mwanza ameapa kupambana kufa na kupona kutatua suala sugu la migogoro ya ardhi ambalo limeendelea kuwa kero ndani ya wilaya yake akiwaasa pia wananchi wa wilaya ya Ilemela kufuata utaratibu wote stahili hasa linapokuja suala la ununuzi au umiliki wa ardhi.


Awali vijana wanaomshabikia Meya Henry Matata waliingia viwanjani hapo kwa mbwembwe wakitokea makaburini ambako walishiriki mazishi ya mmoja kati ya mwanamtaa aliyefariki dunia kwa mapenzi ya mola katani humo.



Suala lililovunja rekodi ndani ya mkutano huo wa hadhara ni hatua ya Meya huyo wa Ilemela kupitia CHADEMA kuvunja mipaka ya itikadi za siasa kwa kualika viongozi na wanachama wa vyama vyote huku akiwaachia kujimwaga na sare zao na hata nyimbo zao za vyama vyao ila tu kwa masharti ya kutohusisha kauli za kubezana zinazoweza kuleta chokochoko hali inayoweza kupelekea uvunjifu wa amani.





Shabiki nambari moko....


Wataalamu mbalimbali kutoka ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela nao walialikwa kwenye kusanyiko hili kwaajili ya kutoa ufafanuzi wa utekelezaji pindi maswali yapapo tokea..

Meya ameahidi kuendelea kuhamasisha wananchi wa Kata ya Kitangiri kushiriki kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia ujenzi wa shule za sekondari hivyo kuondoa uhaba wa vyumba vya madarasa unaoziandama shule nyingi kwa sasa.
                                                                   source:gsengo blog

No comments:

Post a Comment